• HABARI MPYA

  Wednesday, September 22, 2021

  YANGA YAONGOZA KWA MAPATO LIGI KUU


  KLABU ya Yanga ndio imeongoza kuingiza mapato uwanjani katika msimu uliopita wa Ligi Kuu, kiasi Sh.  Milioni 986.8 kutokana na mashabiki 141,681.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu, wanafuatiwa na watani wao, Simba SC walioingiza Milioni 929.7 kutokana na mashabiki 138,518.
  Kwa ujumla Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam ndio umeongoza kwa kuingiza fedha nyingi katika msimu uliopita wa Ligi Kuu, Sh. Bilioni 1.8 ambazo zimetokana na jumla ya mashabiki 274273.
  Taarifa hiyo ya TFF iliyotolewa leo imesema kwamba Uwanja w aCCM Gairo uliopo mkoani Morogoro ndiyo umeshika mkia kwa kuingiza 195,000 kutokana na mashabiki 65 msimu mzima.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAONGOZA KWA MAPATO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top