• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  SIMBA SC WAREJEA DAR KUIVAA MAZEMBE

  KIKOSI cha Simba SC kimerejea Dar es Salaam jana kwa ndege ya Shirika la usafiri wa Anga la Tanzania (ATCL) kutoka Arusha ambako ilipiga kambi ya wiki mbili na ushei kujiandaa na msimu mpya.
  Simba SC watatambulisha rasmi kikosi chao cha msimu mpya kesho kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa mara nne Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Benjamin Mkapa JijininDar es Salaam.
  Huo utakuwa mchezo wa tano wa kirafiki kwa Simba SC baada ya awali kutoka sare mara mbili katika kambi yake ya Jijini Rabat nchini Morocco 2-2 na FAR Rabat na 1-1 na Khourigba, 1-1 na Coastal Union hapo hapo Arusha na kushinda 1-0 dhidi ya Fountain Gate.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA DAR KUIVAA MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top