• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  WAAFRIKA WAING’ARISHA LIVERPOOL ENGLAND

   MABAO ya Waafrika, washambuliaji Msenegal, Sadio Mane dakika ya 43, Mmisri Mohamed Salah dakika ya 78 na kiungo Mguinea, Naby Deco Keita dakika ya 89 yameipa Liverpool ushindi wa 3-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.
  Liverpool imefikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na sasa Inaongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Manchester City iliyocheza mechi tano pia na Manchester United, Chelsea na Everton zenye mechi nne.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAAFRIKA WAING’ARISHA LIVERPOOL ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top