• HABARI MPYA

  Thursday, September 16, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA AC MILAN 3-2

  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AC Milan katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield.
  Liverpool walitangulia kwa bao la Fikayo Tomori dakika ya tisa aliyejifunga baada ya kazi nzuri ya Trent Alexander-Arnold, kabla ya Mohamed Salah kukosa penalti iliyookolewa na kipa Mfaransa, Mike Maignan dakika ya 14.
  AC Milan ikapata mabao mawili mfululizo kupitia kwa Ante Rebic dakika ya 42 na Brahim Diaz dakika ya 44, kabla ya Salah kuisawazishia Liverpool dakika ya 48 na Nahodha Jordan Henderson  kufunga la ushindi dakika ya 69.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA AC MILAN 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top