• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  SIMBA NA GALAXY YA BOTSWANA LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA wa Tanzania, Simba watamenyana na Jwaneng Galaxy FC ya Botswana katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika  mwezi ujao.
  Hiyo ni baada ya Jwaneng Galaxy kuitupa nje Diplomates FC du 8ème Arrondissement, maarufu kama DFC8 ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya kwanza Jijini Gaborone Septemba 11 kabla ya kuchapwa 1-0 jana Jijini Douala.
  Katika mechi ya kwanza nyumbani, mabao ya Jwaneng Galaxy yalifungwa na mshambuliaji Muafrika Kusini, Lucky Nhlanhla Mokoena na kiungo Mnamibia, Wendell Rudath, wakati jana bao pekee la DFC8 lilifungwa na kiungo Delphin Mokonou.


  Simba SC wataanzia ugenini Oktoba 15 Gaborone kabla ya kumalizia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Oktoba 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA GALAXY YA BOTSWANA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top