• HABARI MPYA

  Monday, September 13, 2021

  LIBERPOOL YAICHAPA LEEDS UNITED 3-0

   TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Leeds United usiku wa Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Elland Road.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 20, hilo likiwa bao lake la 100 katika Ligi Kuu ya England, Fabinho dakika ya 50 na Sadio Mane dakika ya 90 na ushei, huku Leeds ikimaliza pungufu baada ya Pascal Struijk kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja moja dakika ya 60 kwa kumchezea rafu Harvey Elliot kufuatia kuingia dakika ya 33 kuchukua nafasi ya Diego Llorente.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 10 sawa na Manchester United na Chelsea baada ya wote kucheza mechi nne sasa wakifuatana nafasi tatu za juu, wakati Leeds inabaki na pointi zake mbili za mechi nne pia katika nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIBERPOOL YAICHAPA LEEDS UNITED 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top