• HABARI MPYA

  Friday, September 17, 2021

  YANGA KUTANGAZA UTALII WA NCHI NIGERIA


  KLABU ya Yanga leo imeingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii kuvaa jezi zenye nembo ya kuutangaza utalii wa nchi kwenye michuano ya Afrika.
  Katika makubaliano hayo, Yanga watavaa jezi za Visit Kilimanjaro & Zanzibar kwenye mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United Jumapili Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
  Yanga SC wanatakiwa kushinda angalau 2-0 ili kusonga mbele baada ya kuchapwa 1-0 Jumapili iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kama Yanga wataweza na wao kushinda 1-0 ugenini, mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUTANGAZA UTALII WA NCHI NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top