• HABARI MPYA

  Thursday, September 23, 2021

  BILIONI 22.8 JENGO LA WIZARA YA MICHEZO

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameridhia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kujengewa jengo jipya Jijini Dodoma.
  Taarifa ya Wizara imesema jengo hilo litagharimu fedha za Kitanzania, Sh. Bilioni 22.843 na litakuwa makao makuu jijini Dodoma.
  Taarifa hiyo imeongeza kwamba tayari mkataba wa ujenzi wa jengo hilo umesainiwa leo kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


  “Hakika hii ni thamani kubwa kwa sekta hizi na jengo hili ni la kwanza kubwa na la thamani zaidi na kali zaidi tangu kuasisiwa kwa sekta hizi kabla na baada ya Uhuru,” imesema taarifa ya Wizara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BILIONI 22.8 JENGO LA WIZARA YA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top