• HABARI MPYA

  Monday, September 27, 2021

  POULSEN AMREJESHA MKUDE TAIFA STARS

  KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wake wa tatu wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Benin Oktoba 7 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika kikosi hicho, Mdenmark huyo amemrejesha kiungo wa Simba SC, Jonas Gerlad Mkude na kumtema Salum Abubakr ‘Sure Boy’ wa Azam FC.


  Kikosi kamili kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Polisi), Wilbol Maseke (Azam), Ramadhani Kabwili (Yanga).
  Mabeki; Israel Mwenda (Simba), Kennedy Juma (Simba), Mohammed Hussein (Simba), Erasto Nyoni (Simba), Dickson Job (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Edward Manyama (Azam FC) na Nickson Kibabage (KMC). 
  Viungo; Meshack Mwamita (kagera Sugar), Novatus Dismas (Maccabu Tel Aviv/Israel), Muzamil Yassin (Simba), Jonas Mkude (Simba) na Feisal Salum (Yanga
  Washambuliaji; John Bocco (Simba), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam), Abdul Suleiman (Coastal Union), Mbwana Samatta (Royal Antwerp/Ubelgiji), Relliant Lusajo (Namungo FC) na Simon Msuva (Wydad AC/Morocco).


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POULSEN AMREJESHA MKUDE TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top