• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  AZAM FC YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO
   TIMU ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Horseed ya Somalia jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Azam FC katika mchezo huo wa marudiano Raundi ya Awali limefungwa na kiungo Ismail Aziz Kada dakika ya 38 na kwa matokeo hayo wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla 4-1 kufuatia kuichapa Horseed 3-1 kwenye mechi ya kwanza hapo hapo Chamazi Jumamosi iliyopita na sasa itakutana na Pyramids ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top