• HABARI MPYA

  Wednesday, September 29, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA PORTO 5-1 URENO


  WENYEJI, FC Porto jana wamechapwa mabao 5-1 na Liverpool katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto, Ureno.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah mawili, dakika ya 18 na 60, Sasio Mané dakika ya 45 na Roberto Firmino mawili pia, dakika ya 77 na 81, wakati la Porto lilifungwa na M. Taremi dakika ya 74.
  Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe pointi sita na kuendelea kuongoza kundi mbele ya Atletico Madrid yenye pointi nne, wakati Porto inabaki na pointi yake moja katika nafasi ya tatu mbele ya AC Milan ambayo haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA PORTO 5-1 URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top