• HABARI MPYA

  Wednesday, September 15, 2021

  YANGA KWENDA NIGERIA KWA NDEGE YA KUKODI

   VIGOGO, Yanga SC wataondoka Ijumaa kwa ndege ya kukodi kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United.
  Katika ndege hiyo ya Shirika la Tanzania, ATCL - Yanga imetoa nafasi pia kwa mashabiki kusafiri kwa gharama ya dola 1200 Economy na 2200 Business.


  Taarifa ya Yanga imesema; "Yanga wanawaalika wanachama wapenzi na mashabiki kujumuika pamoja katika safari ya kwenda kupindua meza Kibabe huko Nigeria.
  Gharama ya safari ni USD 1, 200 kwa daraja Economy na USD 2,200 kwa daraja la Business ikijumuisha pia vipimo vya Covid-19 Dar na Nigeria. Safari ni Ijumaa September 17 na kurudi ni Jumapili Septemba 19, usafiri ni  Airbus A 220-300, Air Tanzania,".
  Baada ya kuchapwa 1-0 Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Yanga watatakiwa kushinda 2-0 Jumapili kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
  Kama watashinda 1-0 mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KWENDA NIGERIA KWA NDEGE YA KUKODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top