• HABARI MPYA

  Tuesday, September 14, 2021

  TP MAZEMBE KUJA NA 23 KUIVAA SIMBA SC

  UONGOZI wa Simba SC umetaja kikosi cha wachezaji 23 cha TP Mazembe ya DRC kitakachowasili Jumamosi kuja kwa ajili ya mchezo wa kirafiki Jumapili wiki hii kwenye tamasha la Simba Day.
  Kwa upande wao, Simba SC bado wanaendelea na mazoezi katika kambi yao ya Arusha kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na kitarajea Ijumaa.
  Huo utakuwa mchezo wa tano wa kirafiki baada ya awali kutoka tatu mara mbili, 2-2 na FAR Rabat na 1-1 na Khourigba katika kambi yake ya Jijini Rabat nchini Morocco, 1-1 na Coastal Union na kushinda mechi moja, 1-0 dhidi ya Faountain Gate katika kambi ya Arusha.


  Ikumbukwe mabingwa hao,wa Tanzania, Simba SC wataanzia hatua inayofuata katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kumenyana na mshindi kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana na DFC 8 ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. 
  Maandalizi haya yataisaidia timu katika mchezo wake wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC Septemba 25 Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TP MAZEMBE KUJA NA 23 KUIVAA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top