• HABARI MPYA

  Wednesday, September 29, 2021

  MWANAHAMISI ANG’ARA, TWIGA YASHINDA COSAFA


  MSHAMBULIAJI Mwanahamisi Omary Shaluwa leo amechaguliwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Zimbabwe akiiwezesha Tanzania kushinda 3-0 katika mchezo wa Kundi B michuano ya COSAFA Uwanja wa Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini.
  Mwanahamisi ‘Gaucho’ anayechezea klabu ya Chabab Atlas Khenifra ya Morocco leo ameifungia Twiga Stars bao la pili dakika ya 60, baada ya Deonisia Minja kufunga la kwanza dakika ya 41 na kabla ya Aisha Masaka kufunga la tatu dakika ya 90 na ushei.
  Twiga Stars itateremka tena dimbani Oktoba 2 kumenyana na Botswana kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Susan Kusini Oktoba 4.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANAHAMISI ANG’ARA, TWIGA YASHINDA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top