• HABARI MPYA

  Saturday, September 25, 2021

  YANGA YAICHAPA SIMBA 1-0 BAO LA MAYELE


  BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii jioni hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam.
  Mayele aliyesajiliwa msimu huu kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa alifunga bao hilo dakika ya 11 akimalizia pasi nzuri ya kiungo mzawa, Farid Mussa Malik.
  Simba SC, washindi wa Ngao kwa misimu minne mfululizo iliyopita walimaliza pungufu baada ya kiungo wao Mganda, Thadeo Lwanga kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu kiungo Mzanzibari wa Yanga, Feisal Salum.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA SIMBA 1-0 BAO LA MAYELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top