• HABARI MPYA

  Tuesday, September 21, 2021

  KIINGILIO CHA CHINI NGAO SH. 10,000

   KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh. 10,000.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), waandaaji wa mechi hiyo imesema viingilio vingine ni Sh. 30, 000 VIP B na 20,000 VIP C na Viti vya Rangi ya Chungwa.
  Mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya, hukutanisha bingwa wa Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na bingwa wa Ligi Kuu.
  Kwa sababu Simba SC walibeba mataji yote hayo msimu uliopita wanakutanishwa na mahasimu wao, Yanga waliomaliza nafasi ya pili katika mashindano hayo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI NGAO SH. 10,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top