• HABARI MPYA

  Sunday, September 19, 2021

  BAYERN MUNICH YASHINDA 7-0 BUNDESLIGA

  TIMU ya Bayern Munich imeendeleza ubabe katika Bundesliga baada ya kuichapa VFL Bochum 7-0 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mabao ya kikosi cha Julian Nagelsmann yakifungwa na Leroy Sane dakika ya 17, Joshua Kimmich mawili dakika ya27 na 64, Serge Gnabry dakika ya32, Vasilios Lampropoulos aliyejifun dakika ya 43, Robert Lewandowski dakika ya 61 na Eric Maxim Choupo-Moting dakika ya79.
  Ushindi huo unaifanya Bayern Munich ifikishe pointi 13 katika mchezo wa tano na kuongoza Bundesliga kwa pointi moja zaidi ya Wolfsburg iliyocheza mechi nne na leo inaikaribisha Eintracht Frankfurt.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH YASHINDA 7-0 BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top