• HABARI MPYA

  Thursday, September 09, 2021

  SIMBA QUEENS MIKONO MITUPU KOMBE LA SAMIA


  TIMU ya Simba Queens imechapwa mabao 2-1 na Lady Doves WFC ya Uganda katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa wanawake, maarufu kama CECAFA Women's Samia Cup mchana wa leo Uwanja wa Moi Kasarani Jijini nchini Kenya.
  Kwa kumaliza nafasi ya tatu, Lady Doves watapata dola za Kimarakani 10,000 wakati bingwa atapata dola 30,000 na mshindi wa pili dola 20,000 sehemu ya dola 100,000 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu Hassan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS MIKONO MITUPU KOMBE LA SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top