// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LEWIS MPYA AKATAA OFA YA MAHELA YA MPINZANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LEWIS MPYA AKATAA OFA YA MAHELA YA MPINZANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 03, 2014

    LEWIS MPYA AKATAA OFA YA MAHELA YA MPINZANI

    BONDIA Anthony Joshua anayetabiriwa kuwa Lennox Lewis mpya, amegoma kukubali ahadi ya kupewa fedha kwa hisani na mpinzani wake Kevin Johnson kuelekea pambano lao mwaka mpya.
    Mmarekani huyo, ambaye hajapigwa katika mapambano yake 36, alitoa ofa ya kumpa asilimia 50 ya pato lake mpinzani wake huyo, Joshua iwapo atashinda.
    Lakini Muingereza Joshua hakuwa tayari kukubali ofa hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari. 
    Anthony Joshua and Kevin Johnson square up at a press conference on Wednesday
    Anthony Joshua na Kevin Johnson wakitunishiana vifua katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo

    Wawili hao watapanda ulingoni kwenye ukumbi wa O2 mjini London Januari 31 ambalo linatarajiwa kuwa pambano gumu kwa Joshua tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa.
    Johnson alipigana na Vitali Klitschko mwaka 2009 na wote Dereck Chisora na Tyson Fury walishindwa kufurukuta mbele yake.
    Johnson amesema: "Nataka kuweka makubaliano na yeye. Ikiwa Anthony atanipiga, nitachangia asilimia 50 ya pato langu kwake kwa hisani,". 
    Johnson na Joshua wakiwa wamepozi na promota Eddie Hearn katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini London
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEWIS MPYA AKATAA OFA YA MAHELA YA MPINZANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top