• HABARI MPYA

  Monday, October 03, 2022

  AZAM FC YAIZIMA SINGIDA STARS 1-0 CHAMAZI


  BAO pekee la Israel Sospeter Bajana dakika ya 45 na ushei limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Azam FC inafikisha pointi 11 katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya nne, wakati Singida Big Stars inabaki na pointi zake nane za mechi tano nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIZIMA SINGIDA STARS 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top