• HABARI MPYA

  Sunday, October 16, 2022

  YANGA ‘OUT’ LIGI YA MABINGWA, YAANGUKIA SHIRIKISHO


  TIMU ya Yanga imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Al Hilal katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora leo Uwanja wa Al Hilal mjini Omdurman nchini Sudan.
  Bao lililoizamisha Yanga limefungwa na Mohamed Abdelhaman dakika tatu ya mchezo huo na kwa matokeo hayo Hilal wanakwenda Hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Dar es Salaam.
  Yanga wao watakwenda kujaribu bahati yao kwa kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA ‘OUT’ LIGI YA MABINGWA, YAANGUKIA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top