• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2022

  RASMI AZAM TV KUONYESHA MECHI YA AL HILAL NA YANGA SUDAN


  HATIMAYE AzamTv imethibitisha kuonyesha 
  mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Al Hilal na Yanga Jumapili Jijini Khartoum nchini Sudan.
  Mechi hiyo inatarajiwa kuanza Saa 3:00 usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia chaneli ya AzamSports1HD.
  Yanga inahitaji ushindi wa ugenini kufuzu Hatua ya makundi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Haitakuwa mara ya kwanza Yanga kujikuta katika mtego wa kupigania ushindi ugenini – kwani mwaka 2001 katika michuano hii na hatua kama hii, Yanga ilitoa sare ya 2-2 na Highlanders FC ya Zimbabwe Jijini Dar es Salaam.
  Lakiki ikafanikiwa kushinda 2-1 Bulawayo katika mchezo wa marudiano mna kusonga mbele, ambako ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 6-5.
  Dhidi ya Mamelodi, Yanga ilifungwa 3-2 Johannesburg kabla ya kulazi na sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI AZAM TV KUONYESHA MECHI YA AL HILAL NA YANGA SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top