• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2022

  HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 3-1


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Man City yalifungwa na Erling Haaland mawili dakika za 22 na 43 kwa penalti na Kevin De Bruyne dakika ya 75, wakati la Brighton limefungwa Leandro Trossard dakika ya 53.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 26 katika mchezo wa 11, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao,  Brighton & Hove Albion wanabaki na pointi zao 15 za mechi 11 pia nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top