• HABARI MPYA

  Wednesday, October 26, 2022

  GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 UHURU


  TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Geita Gold leo yote yamefungwa na viungo wa zamani wa Yanga SC, Juma Mahadhi dakika ya nane na Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 68, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Abalkassim Suleiman dakika ya 20.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold imefikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top