• HABARI MPYA

    Friday, October 28, 2022

    PARIMATCH YAFANYA MABORESHO, YAJA KIBABE NA MFUMO MPYA


    KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha Parimatch imefanya maboresho makubwa katika tovuti yao ya kubashiri, ambayo kwa sasa itawawezesha wateja wao kusuka mikeka yao na ku-share kwa marafiki zao huku wakiwa wanatumia intaneti kidogo wakati wa kuperuzi na kasi kubwa.
    Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizundua rasmi jukwaa hilo la kubashiri mtandaoni kupitia PARIMATCH na kusema kwamba imekuwa ni desturi yao kusikiliza maoni ya wateja wao kila mara na kuamua kuyafanyia uamuzi ili kusudi waweze kuwapatia kitu kilichokuwa bora wateja wao ambao hutumia muda wao ziada kujiburudisha akili zao na Parimatch.
     
    “Tumefanya mabadiliko mazuri, tumerekebisha mambo mengi. Katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika michuano mikubwa ya Kombe la Dunia sisi kama Parimatch, tumeona wateja wetu wanastahili kupata kitu kizuri chenye speed ya uhakika ili wanapokuwa wanapata burudani basi na beti zao ziendane na kasi ya mchezo”, amesema Ismael.
     
    “Licha ya kwamba tumebadilisha tovuti yetu kwa sasa lakini wateja wetu wote watatumia taarifa zao za zamani kuingia www.parimatch.co.tz na wataiona Platform yetu mpya yenye muonekano wa kijanja na wenye kuvutia kwa hakika”
     
    Aidha, Ismael amesema katika maboresho hayo ambayo Parimatch imefanya katika kipindi hiki, yataweza kuwaruhusu watumiaji wa simu za android kuitumia kwa njia ya application kwa urahisi na ufanisi mkubwa zaidi.
    Pamoja na hayo, Ismael pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kukuburudisha na kusisimua.
     
    Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni kwenye kasino na michezo ya virtual, Parimatch ipo zaidi ya nchi 15 duniani kote ikiwa na mamilioni ya wateja. 
     
    Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye michezo, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PARIMATCH YAFANYA MABORESHO, YAJA KIBABE NA MFUMO MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top