• HABARI MPYA

  Monday, October 03, 2022

  YANGA YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 DAR


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 52 na beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 71, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na beki Rolland Msonjo dakika ya 86.
  Kwa matokeo hayo, Yanga wanafikisha pointi 13, ingawa wanabaki nafasi ya pili nyuma ya watani, Simba SC wanaoongoza kwa wastani mzuri tu wa mabao baada ya wote kucheza mechi sita.
  Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao tisa za mechi sita pia nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top