• HABARI MPYA

  Wednesday, October 26, 2022

  YANGA YAICHAPA KMC 1-0 BAO PEKEE LA FEI TOTO


  BAO la kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah dakika ya 80 limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa saba na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 za mechi tisa na Simba pointi 14 za mechi sita.
  KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 13 za mechi tisa nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA KMC 1-0 BAO PEKEE LA FEI TOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top