• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2022

  SALAH APIGA HAT TRICK LIVERPOOL YASHINDA 7-1 UGENINI


  TIMU ya Liverpool jana imeibuka na ushindi wa mnono wa mabao 7-1 dhidi ya wenyeji, Rangers FC katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Ibrox Jijini Glasgow nchini Scotland.
  Rangers walianza vizuri kwa bao la Scott Arfield dakika ya 17, lakini Liverpool ikazinduka kwa mabao ya Roberto Firmino dakika ya 24 na 55, Darwin Núñez dakika ya 66, Mohamed Salah matatu dakika ya 75, 80 na 81 na Harvey Elliott dakika ya 87.
  Liverpool inafikisha pointi tisa baada ya ushindi huo, ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya Napoli inayoongoza kwa pointi zake 12, wakati Rangers inaendelea kushika mkia ikiwa haina pointi, huku Ajax yenye pointi tatu ni ya tatu baada ya wote kucheza mechi nne.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH APIGA HAT TRICK LIVERPOOL YASHINDA 7-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top