• HABARI MPYA

  Saturday, October 29, 2022

  AZAM FC YALETA KOCHA MPYA WA MAZOEZI YA VIUNGO


  MTUNISIA. Dk. Moadh Hiraoui amewasili kuwa Kocha mpya wa mazoezi ya viungo katika klabu ya Azam FC.
  Dk. Moadh Hiraoui. mwenye wasifu mkubwa, amewahi kufanya kazi na vigogo wa Afrika, Esperance ya Tunisia na Al Hilal ya Sudan.
  Hiraoui mwenye PhD ya Sayansi ya Michezo na Afya, pia amewahi kufanya kazi Falme za Kiarabu (UEA) katika timu ya Dibba Al-Hisn na Hajer FC ya Saudi Arabia.
  Tayari mtaalamu huyo ameshaanza kazi, akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongeza.
  Moadh, anachukua nafasi ya Mikel Guillen, ambaye kwa sasa hayupo tena na klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALETA KOCHA MPYA WA MAZOEZI YA VIUNGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top