• HABARI MPYA

  Thursday, October 06, 2022

  SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA CECAFA U17


  TANZANIA imeanza vyema michuano ya CECAFA U17 baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Ethiopia leo katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.
  Mabao ya Tanzania, Serengeti Boys yamefungwa na Sylvester Otto mawili dakika ya tatu na 16 na  Idrisa Makwepa dakika ya 86 na sasa vijana hao watateremka tena dimbani Jumapili kukamilisha mechi zao za Kundi hilo kwa kumenyana na Somalia.
  Ikumbukwe Kundi B linaundwa na Uganda, Burundi na Sudan Kusini na bingwa wa michuano hiyo atashiriki AFCON U17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA CECAFA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top