• HABARI MPYA

  Monday, October 10, 2022

  RONALDO AFUNGA BAO LA 700 MAN U YASHINDA 2-1


  MSHAMBULIAJI Mreno, Cristiano Ronaldo ametokea benchi kuifungia Manchester United bao la pili ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Everton leo Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool.
  Ronaldo alifunga dakika ya 44 baada ya kuingia dakika ya 29 kuchukua nafasi ya Anthony Martial aliyeumia, hilo likiwa bao lake la 700 na rekodi katika historia yake.
  Mshambuliaji Mnigeria, Alexander Chuka Iwobi alianza kuifungia Everton dakika ya tano, kabla ya mshambuliaji mpya, Mbrazil Antony Matheus dos Santos kuwasawazishia Mashetani Wekundu dakika ya 15.
  Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Chelsea ya nne katika msimamo wa Ligi, wakati Everton inabaki na pointi zake 10 za mechi tisa nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA BAO LA 700 MAN U YASHINDA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top