• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2022

  AZIZ KI ÁZIMA SHANGWE ZA SIMBA, SARE NA YANGA 1-1


  MECHI ya watani wa jadi, Yanga na Simba imemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, watani hao wa jadi wakigawana pointi katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ni wageni Simba waliotangulia kwa bao la winga Mghana, Augustine Okrah dakika ya 15, kabla ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kuisawazishia Yanga dakika ya 45.
  Kila timu inafikisha pointi 14 baada ya sare hiyo na kuendelea kufungana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya wote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZIZ KI ÁZIMA SHANGWE ZA SIMBA, SARE NA YANGA 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top