• HABARI MPYA

  Sunday, October 09, 2022

  SIMBA YAWAPIGA WAANGOLA 3-1 KWAO LIGI YA MABINGWA


  TIMU ya Simba imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia Hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Primiero de Agosto leo Uwanja wa Novemba 11 mjini Luanda nchini Angola.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya nane, beki Mzawa, Israel Mwenda dakika ya 63 na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya 76, wakati la Agosto limefungwa na Dago dakika ya 78.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo, Oktoba 16 na mshindi wa jumla atakwenda Hatua ya makundi, wakati timu itakayofungwa itakwenda kuwania kucheza makundi ya Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWAPIGA WAANGOLA 3-1 KWAO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top