• HABARI MPYA

  Sunday, October 30, 2022

  NGORONGORO YAANZA VIBAYA KUWANIA TIKETI YA AFCON U20


  TIMU Taifa ya Tanzania chini ya Umri wa Miaka 20, Ngorongoro Heroes jana ilianza vibaya michuano ya kuwania kufuzu AFCON U20 baada ya kuchapwa 2-0 na Uganda katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.
  Ngorongoro Heroes itateremka tena dimbani Novemba 2 kumenyana na Ethiopia kukamilisha mechi zake za Kundi B ikihitaji lazima ushindi mzuri ili iende Nusu Fainali.
  Ikumbukwe Kundi A linaundwa na Djibouti, Burundi, Sudan Kusini na Sudan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO YAANZA VIBAYA KUWANIA TIKETI YA AFCON U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top