• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2022

  SHAKHTAR YAIKOMALIA REAL MADRID, SARE 1-1 UKRAINE


  WENYEJI, Shakhtar Donetsk wametoka sare ya kufungana bao 1-1 na Real Madrid katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Józefa Piłsudskiego Jijini Warszawa nchini Ukraine.
  Shakhtar Donetsk walitangulia na bao la Oleksandr Zubkov dakika ya 46, kabla ya beki Mjerumani, Antonio Rudiger kuisawazishia Real Madrid dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Real Madrid inafikisha pointi 10 na kuendelea kuongoza kundi kwa pointi nne zaidi ya RB Leipzig wakati Shakhtar Donetsk sasa ina pointi tano nafasi ya tatu mbele ya Celtic yenye pointi moja baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAKHTAR YAIKOMALIA REAL MADRID, SARE 1-1 UKRAINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top