• HABARI MPYA

  Sunday, October 16, 2022

  IHEFU HATIMAYE YASHINDA MECHI YA KWANZA LIGI KUU


  TIMU ya Ihefu imepata ushindi wa kwanza wa msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia kuichapa Dodoma Jiji 2-0 leo Uwanja wa Highlands Estate huko Mbarali, Mbeya.
  Mabao ya Ihefu yamefungwa na Jaffary Kibaya dakika ya 23 na Obrey Chirwa dakika ya 27 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya 14, wakati Dodoma Jiji inayobaki na pointi tano baada ya wote kucheza mechi saba inashukia nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU HATIMAYE YASHINDA MECHI YA KWANZA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top