• HABARI MPYA

  Thursday, October 20, 2022

  MAN UNITED YAIPIGA SPURS 2-0, RONALDO AZÚA JAMBO


  WENYEJI, Manchester United jana waliichapa Tottenham Hotspur mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yalifungwa na Fred dakika ya 47 na Bruno Fernandes dakika ya 69 na kwa ushindi huo Mashetani Wekundu wanafikisha pointi 19 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya tano, wakati Spurs inabaki na pointi 23 za mechi 11 nafasi ya tatu.
  Kocha Mholanzi, Erik ten Hag alistaajabishwa na kitendo cha mshambuliaji Mreno, Cristiano Ronaldo aliyetulizwa benchi jana kuondoka kabla ya mechi kumalizika baada ya kuona muda unayoyoma naye hapewi nafasi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAIPIGA SPURS 2-0, RONALDO AZÚA JAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top