• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2022

  POLISI YAZINDUKA, YAICHAPA NAMUNGO 1-0 MOSHI


  TIMU ya Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Kilimanjaro.
  Bao pekee la Polisi Tanzania limefungwa na Rajab Athumani dakika ya 40 na kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu wanafikisha pointi tano katika mchezo wa nane nafasi ya 15.
  Kwa upande wao, Namungo FC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 11 za mechi sita nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI YAZINDUKA, YAICHAPA NAMUNGO 1-0 MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top