• HABARI MPYA

  Sunday, October 30, 2022

  ARSENAL YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 5-0 EMIRATES


  TIMU ya Arsenal imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Nottingham Forest mabao 5-0 leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Martinelli dakika ya tano, Reiss Nelson mawili dakika ya 49 na 52, Thomas Partey dakika ya 57 na Martin Odegaard dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 31 na kurejea kileleni ikiizidi pointi mbili Manchester City baada ya wote kucheza mechi 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 5-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top