• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2022

  AZAM FC YAACHANA NA KOCHA WAKE MFARANSA MAPEMA TU


  KLABU ya Azam FC imeachana na kocha wake Mfaransa, Denis Lavagne baada ya mwezi mmoja na ushei tangu aajiriwe.
  Hatua hiyo inakuja baada ya Azam FC kuchapwa 2-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Ijumaa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Lavagne mwenye leseni ya UEFA Pro,  alijiunga na Azam FC Septemba 2, mwaka huu akichukua nafasi ya Msomali, Abdihamid Moalin aliyefukuzwa mwishoni mwa mwezi Agosti.
  Sasa timu itakuwa chini ya Muingereza mwenyeji nchini, Kali Ongala na Waspaniola, Dani Cadena kocha wa makipa, Mikel Guillen kocha wa Fiziki na mtaalamu wa tiba za wanamichezo (physio), Mreno Joao Rodrigues.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAACHANA NA KOCHA WAKE MFARANSA MAPEMA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top