• HABARI MPYA

  Wednesday, October 26, 2022

  CHELSEA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA


  TIMU ya Chelsea imefanikiwa kufuzu Hatua ya Mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Red Bull Salzburg katika mchezo wa Kundi E usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena mjini Wals-Siezenheim nchini 
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Mateo Kovacic dakika ya 23 na Kai Havertz dakika ya 64, wakati la Red Bull Salzburg limefungwa na Junior Adamu dakika ya 49.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 10 na kuendelea kuongoza Kundi kwa pointi tatu zaidi ya AC Milan wanaofuatia mbele ya Red Bull Salzburg yenye pointi sita baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top