• HABARI MPYA

  Saturday, October 22, 2022

  NOTTINGHAM YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 CITY GROUND


  TIMU ya Nottingham Forest imepata ushindi wa kwanza tangu mwezi Agosti baada ya kuwalaza Liverpool 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa City Ground, Nottingham, Nottinghamshire.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mnigeria Taiwo Awoniyi dakika ya 55 aliyeifunga timu yake ya zamani aliyoitumikia kwa miaka sita.
  Kwa ushindi huo kikosi cha Steve Cooper kinafikisha pointi tisa katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya 19, ikiizidi pointi moja Leicester City ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao vijana wa Jurgen Klopp wanabaki na pointi zao 16 za mechi 11 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NOTTINGHAM YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 CITY GROUND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top