• HABARI MPYA

  Friday, October 28, 2022

  RONALDO AREJEA NA KUFUNGA MAN U YASHINDA 3-0 ULAYA


  TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Hatua ya Mtoano ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi E usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na beki Diogo Dalot dakika ya 44 na washambuliaji, Marcus Rashford dakika ya 65 na Cristiano Ronaldo dakika ya 81 na kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 12, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tatu na vinara, Real Sociedad.
  Mashetani hao Wekundu watahitaji kushinda mabao mawili bila kuruhusu bao dhidi ya timu ya LaLiga, Real Sociedad katika mchezo wa mwisho ili kumaliza kileleni mwa Kundi lao, E.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AREJEA NA KUFUNGA MAN U YASHINDA 3-0 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top