• HABARI MPYA

  Thursday, October 06, 2022

  REAL MADRID YAICHAPA SHAKHTAR 2-1 HISPANIA


  WENYEJI, Real Madrid wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mchezo wa Kundi F usiku wa jana Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Rodrygo dakika ya 13 na Vinicius Junior dakika ya 28, la  Shakhtar Donetsk likifungwa na Oleksandr Zubkov dakika ya 39.
  Kwa ushindi huo, Real Madrid wanafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tano zaidi ya  Shakhtar Donetsk.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA SHAKHTAR 2-1 HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top