• HABARI MPYA

  Tuesday, October 25, 2022

  PRISONS YAIKANDAMIZA POLISI 2-0 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jeremiah Juma kwa penalti dakika ya tano na Samson Mbangula dakika ya 45 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya sita.
  Kwa upande wao Polisi Tanzania wanabaki na pointi zao tano baada ya kucheza mechi tisa sasa ikihamia mkiani mwa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAIKANDAMIZA POLISI 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top