• HABARI MPYA

  Tuesday, October 25, 2022

  NAMUNGO FC YAIKANDAMIZA KAGERA SUGAR 2-1 MAJALIWA


  WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya nane na Jacob Massawe dakika ya 67, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka Yussuf dakika ya 45 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake nane za mechi tisa sasa nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAIKANDAMIZA KAGERA SUGAR 2-1 MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top