• HABARI MPYA

  Thursday, October 06, 2022

  RASHFORD APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-2 CYPRUS


  WENYEJI, Omonia Nicosia wameiruhusu Manchester United kupata ushindi wa ugenini wa 3-2 leo katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League Uwanja wa Neo GSP Jijini Nicosia, Cyprus.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford mawili dakika ya 53 na 84 na Anthony Martial dakika ya 63, wakati ya Omonia Nicosia yamefungwa na Karim Ansarifard dakika ya 34 na Nikolaos Panagiotou dakika ya 85.
  Kwa matokeo hayo, Manchester United wanafikisha pointi sita, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tatu na Real Sociedad baada ya wote kucheza mechi tatu. 
  Omonia Nicosia inaendelea kushika mkia ikiwa haina pointi, nyuma ya Sheriff yenye pointi tatu kufuatia kila timu katika kundi hilo kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASHFORD APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-2 CYPRUS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top