• HABARI MPYA

  Wednesday, October 26, 2022

  POLISI TANZANIA YAACHANA NA KOCHA WAKE MFARANSA


  KLABU ya Polisi Tanzania imeachana na kocha wake Mrundi, Joslin Sharrif Bipfubusa baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na timu hiyo Julai 26.
  Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Polisi Tanzania kuchapwa 2-0 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kwa ujumla mwenendo wa Polisi haukuwa mzuri chini ya Bipfubusa, kwani katika mechi tisa ilizocheza hadi sasa imeambulia pointi tano tu kufuatia kushinda moja na sare mbili, huku nyingine zote sita ikipoteza.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAACHANA NA KOCHA WAKE MFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top