• HABARI MPYA

  Sunday, October 30, 2022

  MAN CITY YAIBAMIZA LEICESTER CITY 1-0


  BAO pekee la Kevin De Bruyne dakika ya 49 jana liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power, Leicester, Leicestershire. 
  Kwa ushindi huo, kikosi cha Pep Guardiola kinarejea kileleni japo kwa muda kufuatia kufikisha pointi 29 katika mchezo wa 12, wakiizidi pointi moja Arsenal ambayo ina mechi moja mkononi.
  Hali bado si nzuri kwa kocha Brendan Rodgers, kwani baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 sasa nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA LEICESTER CITY 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top