• HABARI MPYA

  Monday, October 31, 2022

  DUBE TENA, AZAM FC YASHINDA 1-0 TENA LIGI KUU DAR


  BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 55 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya tatu, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake tano za mechi tisa nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DUBE TENA, AZAM FC YASHINDA 1-0 TENA LIGI KUU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top